• Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia. [Zaburi 5:11]
  • Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele. [Zaburi 16:11]
  • Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha. [Zaburi 30:5]
  • Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. [Zaburi 126:5]
  • Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema. [Zaburi 128:1, 2]
  • Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia. [Isaya 35:10]
  • Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. [Yohana 15:11]
  • Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.[Warumi 14:17]