Thursday, January 29, 2015

USALAMA NA ULINZI

  • Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama. [Mambo ya Walawi 25:18]
  • Akamnena Benyamini, Mpenzi wa Bwana atakaa salama kwake; Yuamfunika mchana kutwa, Naye hukaa kati ya mabega yake. [Kumbukumbu la Torati 33:12]
  • basi, sasa, uwe radhi, ukaibarikie nyumba ya mtumwa wako, ipate kudumu milele mbele zako; kwa maana wewe, Ee Bwana MUNGU, umelinena na kwa baraka yako nyumba ya mtumwa wako na ibarikiwe milele. [2 Samweli 7:29]
  • Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda. [2 Samweli 8:6]
  • nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani. [1 Mambo ya Nyakati 17:8]
  • Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa. Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia. Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.[Zaburi 21:7-9]
  • Bali mfalme atamfurahia Mungu, Kila aapaye kwa Yeye atashangilia, Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa. [Zaburi 63:11A]
  • Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu. Adui zake nitawavika aibu, Bali juu yake taji yake itasitawi. [Zaburi 132:17,18]
  • Awapaye wafalme wokovu, Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu. [Zaburi 144:10]

No comments:

Post a Comment