Thursday, January 29, 2015

KUPUMZIKA KATIKA BWANA

  • Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. [Kutoka 33:14]
  • Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu. [1 Samweli 9:27]
  • Naye akawaambia Yuda, Na tuijenge miji hii, na kuizungushia maboma, na minara, na malango, na makomeo; nchi bado ikalipo mbele yetu, kwa kuwa tumemtafuta Bwana, Mungu wetu; naam, tumemtafuta, naye amemstarehesha pande zote. Basi wakajenga, wakafanikiwa. [2 Mambo ya Nyakati 14:7B]
  • Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia. [Zaburi 4:4]
  • Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana. [Zaburi 27:14]
  • Ukae kimya mbele za Bwana, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila. [Zaburi 37:7]
  • Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu. [Zaburi 40:1]
  • Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi. [Zaburi 46:10A]
  • Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.[Zaburi 55:22]
  • Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. [Zaburi 62:8]
  • Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.[Isaya 26:3]
  • Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. [Isaya 30:15B]
  • Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. [Isaya 32:17]
  • bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. [Isaya 40:31]
  • Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. [Yeremia 17:7]
  • Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. [Yeremia 29:11]
  • Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu. [Maombolezo 3:25, 26]
  • Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. [Mathayo 11:28-30]
  • Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.[Wafilipi 4:7]
  • Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.[2 Timotheo 1:12B]
  • huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. [1 Petro 5:7]

No comments:

Post a Comment