- Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. [Yohana 1:1,14]
- Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. [Mathayo 4:4]
- Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. - [Zaburi 119:11]
- Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. - [Yohana 15:3]
- Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga. - [Zaburi 119:130]
- Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. - [2 Timotheo 2:15]
- Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. - [Waebrania 4:12]
- Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. -[Yohana 6:63]
- Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. - [Mathayo 24:35]
- Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; - [1 Petro 2:2]
Karibu sana katika blog hii, Na utapata kujifunza mengi kuhusu biblia huku ukishilikiana na ndugu, jamaa na marafiki kujadili maada mbali mbali za biblia. Kama una swali au maoni yoyote juu ya biblia unaweza kutoka comment yako ili upate majibu kutoka kwa jamaa, ndugu na rafiki zako..
Thursday, January 29, 2015
NENO LA MUNGU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment