Thursday, January 29, 2015

UAMINIFU

  • Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; - [Wakolosai 3:9]
  • Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. - [Warumi 12:17]
  • tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu. - [2 Wakorintho 8:21]
  • Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. - [Mithali 11:1,3]
  • Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu. Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila. - [Mithali 12:13,17]
  • Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. - [Mithali 28:13]
  • Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. - [Yakobo 5:16]
  • lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu. - [2 Wakorintho 4:2]

No comments:

Post a Comment