WAEFESO 6:10-18
10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Biblia inavyo sema vaeni silaha zote za MUNGU, ujue ya kwamba kuna vita, na palipo na vita pia kuna WAPIGANAJI.
Hauwezi kubeba silaha kwaajili ya kufanya vita kama hakuna maadui/wapiganaji maana itakua ni jambo la kushangaza, ndio maaana hata mwandishi wa kitabu hiki(WAEFESO) Paul.. alielezea wazi wazi silaha za MUNGU kwa kanisa kwaajili ya kupigana vita vya KIROHO.
Silaha zilizo tajwa kwenye kitabu cha WAEFESO ni kama zifuatazo...
- KWELI (Yohana 17:17, Waefeso 4:17, 1 Petro 1:22)
- HAKI (Mithali 29:2,6)
- UTAYARI (Isaya 52:7)
- CHAPEO YA WOKOVU (1 Wathesalonike 5:8)
- NENO LA MUNGU (Yoshua 1:8, Zaburi 119:11, Zaburi 150, Timotheo 3:16)
- IMANI (1 Yohana 5:4, Waebrania 11:1)
- MAOMBI YA MUDA MREFU (Luka 18:1, Wakolosai 4:2, Mathayo 26:36-44)
Ndugu yangu katika BWANA nakuomba usome vifungu vyote nilivyo vinakiri katika somo hili, Nina hakika kama ukivisoma hauta baki kama ulivyo kua.. MUNGU akusaidie.
MWISHO. MUNGU atusaidie kushinda maana Shetani kila siku anaongeza mbinu za kuwashinda watu wa MUNGU, kusudi wasifikie lile lengo MUNGU alilo kusudia juu YETU.