Wednesday, January 28, 2015

SOMA BIBLIA AU SIKILIZA BIBLIA KWENYE MTANDAO.

BIBLIA KWA KISWAHILI         BIBLE IN ENGLISH   BIBLE IN ALL LANGUAGE

BIBLIA YA KISWAHILI KWA SAUTI    ENGLISH AUDIO BIBLE   ALL LANGUAGE AUDIO BIBLE    BOFYA HAPA KUPATA VIFUNGU VYA BIBLIA KULINGANA NA MAHITAJI YAKO

CLICK HERE FOR ALL LANGUAGE BIBLE VERSES SELECTION



 BOFYA SEHEMU UNAYO HITAJI HAPO JUU NA USOME AU KUSIKILIZA BIBLIA KWA LUGHA UIPENDAYO.

NI LINI MWISHO WA DUNIA NA NI NINI DALILI ZAKE

MATHAYO 24:3-51

  •  Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?
  •  Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.
  •  Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.
  •  Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.
  •  Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.
  •  Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.
  •  Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
  •  Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.
  •   Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
  •  Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
  •  Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
  •  Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
  •  Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
  •  ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;
  •  naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake;
  •  wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake.
  •  Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo!
  •  Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.
  •  Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
  •  Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
  •  Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.
  •  Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
  •  Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.
  •  Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.
  •  Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
  •  Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
  •  Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
  •  ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
  •  Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.
  •  Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
  •  nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
  •  Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.
  •  Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
  •  Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
  •  Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
  •  Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
  •  wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
  •  Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
  •  wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
  •   Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.
  •  Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
  •  Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.
  •  Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?
  •  Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.
  •  Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
  •  Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;
  •  akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi;
  •  bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,
  •  atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.



AMRI KUU KATIKA BIBLIA

MATHAYO 22:34-40

  •  Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja.
  •  Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
  •  Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
  •  Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
  • Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
  • Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
  • Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

BOFYA HAPA KWA MAELEZO SAIDI KUHUSU USOMAJI WA BIBLIA KWENYE MTANDAO.


NI MAISHA YA NAMNA GANI WATAISHI WATAKATIFU WA MUNGU BAADA YA MAISHA HAYA

MATHAYO 22:23-32

  •   Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,
  •  wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
  •  Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.
  • Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.
  •  Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.
  •  Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
  • Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
  •  Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.
  •  Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema,
  •  Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai.


BOFYA HAPA KUSOMA BIBLIA
BOFYA HAPA KWA MAELEZO SAIDI KUHUSU USOMAJI WA BIBLIA KWENYE MTANDAO.

NI UJIRA GANI ANAPATA YEYOTE AACHAYE YOTE AJILI YA BWANA

MATHAYO 19:27-29

  •  Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
  •  Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
  •  Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.



KUNA UKWELI GANI KUHUSU VYAKULA!!, JE? NI HALALI KULA VYAKULA VYOTE?

MATHAYO 15:10-20

  • Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
  • Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
  • sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
  • Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.

BOFYA HAPA KWA MAELEZO SAIDI KUHUSU USOMAJI WA BIBLIA KWENYE MTANDAO.

ANGALIA SADAKA YAKO NA SALA ZAKO ZISIPITE BURE.

MATHAYO 6:2-5

  •  Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
  •  Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
  •  sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
  •  Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.


BOFYA HAPA KUSOMA BIBLIA
BOFYA HAPA KWA MAELEZO SAIDI KUHUSU USOMAJI WA BIBLIA KWENYE MTANDAO.

KUNA TOFAUTI GANI KATIKA AMRI ZA MUNGU KATI YA AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA?

KUTOKA"OXODUS" 20:1-17  (AGANO LA KALE)

  •  Mungu akanena maneno haya yote akasema,
  • Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
  • Usiwe na miungu mingine ila mimi.
  • Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
  • Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
  • nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
  • Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
  • Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
  • Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
  •  lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
  • Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
  • Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
  •  Usiue.
  •  Usizini.
  •  Usiibe.
  •  Usimshuhudie jirani yako uongo.
  •  Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.




MATHAYO 5:21-48   (AGANO JIPYA)

  •   Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
  •   Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
  •   Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
  •  iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
  •   Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
  •   Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
  •  Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
  •  lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
  • Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
  •  Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
  • Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
  • lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
  •  Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
  •   lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
  •  wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
  •   Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
  •  Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
  •   Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
  •  Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
  •  Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
  • Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.
  •  Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.
  •  Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
  •   lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
  •   ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
  •   Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
  •  Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
  •   Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


MATENDO NA MIENENDO YA WOTE WAMPENDAO BWANA.

MATHAYO 5:3-12
  •  Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
  •  Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.
  •  Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
  •  Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
  •  Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
  •  Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
  •  Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
  •  Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
  •  Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
  •  Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

BOFYA HAPA KUSOMA BIBLIA
BOFYA HAPA KWA MAELEZO SAIDI KUHUSU USOMAJI WA BIBLIA KWENYE MTANDAO.