- Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja.
- Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
- Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
- Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
- Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
- Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
- Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
BOFYA HAPA KWA MAELEZO SAIDI KUHUSU USOMAJI WA BIBLIA KWENYE MTANDAO.
No comments:
Post a Comment