Wednesday, January 28, 2015

NI LINI MWISHO WA DUNIA NA NI NINI DALILI ZAKE

MATHAYO 24:3-51

  •  Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?
  •  Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.
  •  Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.
  •  Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.
  •  Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.
  •  Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.
  •  Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
  •  Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.
  •   Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
  •  Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
  •  Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
  •  Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
  •  Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
  •  ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;
  •  naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake;
  •  wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake.
  •  Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo!
  •  Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.
  •  Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
  •  Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
  •  Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.
  •  Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
  •  Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.
  •  Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.
  •  Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
  •  Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
  •  Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
  •  ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
  •  Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.
  •  Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
  •  nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
  •  Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.
  •  Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
  •  Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
  •  Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
  •  Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
  •  wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
  •  Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
  •  wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
  •   Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.
  •  Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
  •  Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.
  •  Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?
  •  Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.
  •  Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
  •  Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;
  •  akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi;
  •  bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,
  •  atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.



No comments:

Post a Comment