Wednesday, January 28, 2015

KUNA TOFAUTI GANI KATIKA AMRI ZA MUNGU KATI YA AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA?

KUTOKA"OXODUS" 20:1-17  (AGANO LA KALE)

  •  Mungu akanena maneno haya yote akasema,
  • Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
  • Usiwe na miungu mingine ila mimi.
  • Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
  • Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
  • nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
  • Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
  • Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
  • Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
  •  lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
  • Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
  • Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
  •  Usiue.
  •  Usizini.
  •  Usiibe.
  •  Usimshuhudie jirani yako uongo.
  •  Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.




MATHAYO 5:21-48   (AGANO JIPYA)

  •   Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
  •   Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
  •   Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
  •  iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
  •   Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
  •   Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
  •  Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
  •  lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
  • Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
  •  Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
  • Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
  • lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
  •  Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
  •   lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
  •  wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
  •   Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
  •  Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
  •   Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
  •  Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
  •  Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
  • Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.
  •  Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.
  •  Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
  •   lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
  •   ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
  •   Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
  •  Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
  •   Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


No comments:

Post a Comment