- Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
- Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.
- Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
- Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
- Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
- Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
- Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
- Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
- Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
- Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
BOFYA HAPA KWA MAELEZO SAIDI KUHUSU USOMAJI WA BIBLIA KWENYE MTANDAO.
No comments:
Post a Comment