Thursday, January 29, 2015

HEKIMA NA MAAMUZI

  • akawaambia hao makadhi, Angalieni myafanyayo; kwa kuwa hammfanyii mwanadamu hukumu, ila Bwana; naye yupo pamoja nanyi katika neno la hukumu. [2 Mambo ya Nyakati 19: 6B]
  • Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; [Mithali 2:3 , 5, 6]
  • Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana. [Mithali 16:1]
  • Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao Bwana huelewa na yote. [Mithali 28:5]
  • Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; [Isaya 11:2 , 3]
  • Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieliii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto. [Danieli 1:17]
  • Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. [Yakobo 1:5]
  • Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu. [Zaburi 143:8]
  • Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni; [Zaburi 143:10 , 11A]
  • mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.[Mithali 1:5]
  • Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.[Mithali 12:15B]
  • Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika. [Mithali 15:22]
  • Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho. [Mithali 19:20]
  • Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita. [Mithali 20:18]
  • Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu. [Mithali 24:6]
  • Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki. [Yohana 7:24]
  • Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. [Yakobo 3:17]
  • Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa. [2 Wakorintho 13:1B]

No comments:

Post a Comment