Thursday, January 29, 2015

KUPUMZIKA NA LIKIZO

  • Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza. [Zaburi 3:5]
  • Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama. [Zaburi 4:8]
  • Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, [Zaburi 91:5]
  • Yeye humpa mpenzi wake usingizi. [Zaburi 127:2B]
  • Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. [Mithali 3:24]
  • Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au kwamba amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi. [Mhubiri 5:12]
  • Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake.[Isaya 57:2]
  • Na ahimidiwe Bwana, aliyewapa watu wake Israeli kustarehe, vile vile kama yote aliyoyaahidi. Halikukosa kupatikana neno lo lote katika ahadi yake njema, aliyoahidi kwa mkono wa Musa, mtumishi wake. [1 Wafalme 8:56A]
  • Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini; Naam, utatafuta-tafuta kando yako, na kupumzika katika salama. [Ayubu 11:18]
  • Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake.[Isaya 57:2]
  • Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo. [Isaya 58:13,14A]
  • Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. [1 Wakorintho 10:31]
  • Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. [Waebrania 4: 9 , 10]

No comments:

Post a Comment