Thursday, January 29, 2015

KUSIFU

  • Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. [2 Mambo ya Nyakati 20:22]
  • kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. [Nehemia 8:10B]
  • Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu. [Zaburi 50:23]
  • Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe, Ee Bwana, huenenda katika nuru ya uso wako. [Zaburi 89:15]
  • Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge. [Yeremia 30:19]
  • wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. [Matendo ya Mitume 2:47]
  • Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. [Wafilipi 4:6]
  • Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu. [Mathayo 5:10-12]
  • Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo. [Luka 6:22, 23]
  • Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. [Yohana 16:33]
  • Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo. [Matendo ya Mitume 5:41]
  • La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi? [Warumi 9: 20]
  • kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote. [2 Wakorintho 6:10]
  • Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. [Wafilipi4:11B]
  • shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. [1 Wathesalonike 5:18]
  • Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. [Waebrania 10:34]
  • Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, [1 Petro 1:8]
  • Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. [1 Petro 3:14]
  • Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo. [1 Petro 4:13, 16]
  • Mfurahieni Bwana; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo. [Zaburi 32:11]
  • Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. [Zaburi 33:1]
  • Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima. [Zaburi 34:1]
  • Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa. [Zaburi 35:28]
  • Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. [Zaburi 68:19]
  • Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa. [Zaburi 71:8]
  • Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku. [Zaburi 92:1, 2]
  • Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; [Zaburi 100:4]
  • Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. [Zaburi 103:1, 2]
  • Na wamshukuru Bwana, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. [Zaburi 107:8]
  • Na wamtolee dhabihu za kushukuru, Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba. [Zaburi 107:22]
  • Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa. [Zaburi 113:3]
  • Na tumwinulie Mungu aliye mbinguni Mioyo yetu na mikono. [Maombolezo 3:41]
  • Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana. [Yona 2:9]
  • mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; [1 Wathesalonike 5:18]
  • shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. [Waefeso 5:19, 20]
  • Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. [Waebrania 13:15]
  • Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. [Ufunuo wa Yohana 19:5B]

No comments:

Post a Comment