Thursday, January 29, 2015

UKWELI ZAIDI KUMHUSU KRISTO YESU

YOHANA 1:1-18

  • Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
  • Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
  • Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
  • Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
  • Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
  • Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.
  • Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.
  • Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.
  • Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
  •  Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
  •  Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
  • Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
  •  waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
  •  Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
  • Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
  •  Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.
  •  Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
  • Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.



No comments:

Post a Comment